4. Madhabahu ya Uvumba Ni Mahali Ambapo Mungu Anaitoa Neema Yake (Kutoka 30:1-10)

Episode 4 January 24, 2023 00:47:58
4. Madhabahu ya Uvumba Ni Mahali Ambapo Mungu Anaitoa Neema Yake (Kutoka 30:1-10)
HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA (III): Ubainisho wa Injili ya Maji na Roho
4. Madhabahu ya Uvumba Ni Mahali Ambapo Mungu Anaitoa Neema Yake (Kutoka 30:1-10)

Jan 24 2023 | 00:47:58

/

Show Notes

Kama tungeliingia ndani ya Mahali Patakatifu, ambapo ni Nyumba ya Mungu, kitu cha kwanza ambacho tungelikiona ni kinara cha taa, meza ya mikate ya wonyesho, na madhabahu ya uvumba. Madhabahu ya uvumba iliwekwa mbele ya lango la kuingia Patakatifu pa Patakatifu, mahali ambapo kiti cha rehema kilikuwa kimewekwa, yaani baada ya kukipita kinara cha taa na meza ya mikate ya wonyesho. Urefu na upana wa madhabahu hii ya uvumba ulikuwa ni dhiraa moja, wakati kimo chake kilikuwa ni dhiraa mbili. Katika Biblia, dhiraa ni takribani sentimita 45-50 kwa vipimo vya hivi sasa. Hivyo, madhabahu ya uvumba ilikuwa na mraba mdogo wenye vipimo vya takribani sentimita 50 kwa urefu na upana na sentimita 100 kwa kimo. Kama ilivyokuwa kwa madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, madhabahu ya uvumba pia ilikuwa na pembe katika zake nne za juu. Hali ikiwa imetengenezwa kwa mti wa mshita, madhabahu ya uvumba ilikuwa imefunikwa yote kwa dhahabu.

https://www.bjnewlife.org/
https://youtube.com/@TheNewLifeMission
https://www.facebook.com/shin.john.35

Other Episodes

Episode 3

January 24, 2023 00:45:18
Episode Cover

3. Madhabahu ya Sadaka ya Kuteketezwa Iliyotengenezwa Kwa Mti wa Mshita na Kufunikwa Kwa Shaba (Kutoka 38:1-7)

Ili mwenye dhambi yeyote kati ya watu wa Israeli aweze kuondolewa dhambi zake, basi ilimpasa kuleta mnyama wa sadaka ya kuteketezwa katika Hema Takatifu...

Listen

Episode 7

January 24, 2023 00:55:46
Episode Cover

7. Vikombe Vya Mapambo Kwa Injili ya Maji na Roho (Kutoka 25:31-40)

Kifungu hiki kinaelezea juu ya kinara cha taa cha Hema Takatifu la Kukutania. Leo nitapenda kuelezea juu ya maana ya kiroho ya vikombe hivi...

Listen

Episode 5

January 24, 2023 01:06:35
Episode Cover

5. Maana ya Kiroho ya Vikuku vya Fedha Vilivyotumika Katika Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 26:15-30)

Mbao zote za Hema Takatifu la Kukutania mahali ambapo Mungu alikaa zilikuwa zimefunikwa kwa dhahabu. Mungu alimwambia Musa kutengeneza vikuku vya fedha ili kuushikiza...

Listen