Ili mwenye dhambi yeyote kati ya watu wa Israeli aweze kuondolewa dhambi zake, basi ilimpasa kuleta mnyama wa sadaka ya kuteketezwa katika Hema Takatifu la Kukutania, na kisha kuzipitisha dhambi zake juu ya mnyama huyo wa sadaka kwa kuiweka mikono yake juu ya kichwa cha mwanasadaka huyo, na kisha kuikinga damu yake, na kisha kuikabidhi damu hii kwa kuhani. Kuhani aliye katika zamu yake aliiweka damu hii ya mwanasadaka katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, aliyaweka mafuta na nyama ya mwanasadaka huyo juu ya madhabahu, kisha akavichoma vitu hivyo kama manukato mazuri kwa Bwana Mungu. Hata Kuhani Mkuu, ili aweze kupokea ondoleo la dhambi zake, basi alipaswa kuiweka mikono yake juu ya mnyama wa sadaka ya kuteketezwa na kisha kuzipitisha dhambi zake kwa mnyama huyo mbele ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. Hii ilikuwa ni sadaka ya upatanisho iliyokuwa ikitolewa katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa ambayo ilitengenezwa kutokana na mti wa mshita na kisha kufunikwa kwa shaba, na sadaka hii ya ondoleo la dhambi ilitolewa baada ya tendo la kuiweka mikono juu ya mwanasadaka na kisha kuimwaga damu huyo mwanasadaka.
https://www.bjnewlife.org/
https://youtube.com/@TheNewLifeMission
https://www.facebook.com/shin.john.35
Leo hii hebu tuangalie katika kumsimika Kuhani Mkuu. Hapa tunaona kwamba Mungu alimwamuru Musa jinsi yay kumsimika Haruni na wanawe kwa kina. Neno “kusimika”...
Ni Kuhani Mkuu ndiye aliyetoa sadaka katika Siku ya Upatanisho kwa ajili ya watu wa Israeli. Sadaka hii ilitolewa mara moja kwa mwaka siku...
Wigo wa mstahili wa ua wa Hema Takatifu la Kukutania ulikuwa na dhiraa 100 kwa urefu. Katika Biblia, dhiraa moja ulikuwa ni urefu unaoanzia...