Hebu sasa tukiangalie kifuko cha kifuani ambacho Kuhani Mkuu alikitumia katika kuwahukumu watu wa Israeli. Kifungu cha maandiko hapo juu kinatueleza kuwa kifuko cha kifuani cha hukumu kilitengenezwa kwa kitambaa kilichokuwa na mraba unaolingana kwa vipimo kwa urefu na upana wake. Kitambaa hiki kilikuwa kimefumwa kiujuzi kwa nyuzi za dhahabu, za bluu, za zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Vito kumi na mbili vya thamani viliwekwa katika kitambaa hiki huku kila mstari ukiwa na vito vitatu na hivyo kufanya jumla ya mistari minne. Pia Mungu alimwambia Musa kuweka Urimu na Thumimu katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu. Urimu na Thumimu zina maanisha ni ‘mwanga na ukamilifu.’
https://www.bjnewlife.org/
https://youtube.com/@TheNewLifeMission
https://www.facebook.com/shin.john.35
Ili mwenye dhambi yeyote kati ya watu wa Israeli aweze kuondolewa dhambi zake, basi ilimpasa kuleta mnyama wa sadaka ya kuteketezwa katika Hema Takatifu...
Kama tungeliingia ndani ya Mahali Patakatifu, ambapo ni Nyumba ya Mungu, kitu cha kwanza ambacho tungelikiona ni kinara cha taa, meza ya mikate ya...
Mungu anatuonyesha nini kupitia kilemba hiki cha Kuhani Mkuu? Kilemba na yale mapambo yake vina maanisha kwamba Yesu Kristo alizichukua dhambi zetu zote kwa...